Thursday, 14 December 2017
KUITWA KWENYE USAILI
OFISI
YA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA INAPENDA KUWATANGAZIA
KUWA KUTAKUWA NA USAILI SIKU YA TAREHE 18–20/12/2017 KUFUATIA TANGAZO LA NAFASI
YA KAZI YA MTENDAJI KIJIJI DARAJA LA III NA DEREVA – II LILILOTOLEWA TAREHE 28/09/2017 NA 23/11/2017.
KADA ZITAKAZOHUSIKA KATIKA USAILI HUO
NI WATENDAJI WA VIJIJI – III NA DEREVA II KAMA ILIVYOTANGAZWA AWALI, USAILI UTAFANYIKA OFISI YA MKURUGENZI
MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA KWA TAREHE TAJWA HAPO JUU KUANZIA SAA
2:00 ASUBUHI.TAREHE 18/12/2017 UTAFANYIKA USAILI WA
KUANDIKA NA TAREHE 19 HADI 20/12/2017 UTAFANYIKA USAILI WA MAHOJIANO KWA WALE
WATAKAOFAULU USAILI WA KUANDIKA (MTIHANI WA MCHUJO).
TAFADHALI FIKA NA VYETI VYAKO VYOTE HALISI (ORIGINALS) VIKIWEMO CHETI CHA KIDATO CHA NNE, CHETI CHA TAALUMA (CHUO), CHETI CHA KUZALIWA NA TRANSCRIPT.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment