Monday, 8 June 2015

MBINGA YAKAMILISHA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA VITAMBULISHO KWA MAFANIKIO MAKUBWA


Msimamizi wa uchaguzi kata ya Betrehemu   (ARO KATA) , Mr Alphone Njawa akiwa kabeba BVR tayari kwa kwenda kazini wakati wa zoezi la uandikishaji wa vitambulisho yva kupigia kura 2015, Zoezi hilo kwa Wilaya ya Mbinga  limekamilika hivi karibuni

Zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya kupigia kura katika daftari la kudumu la uchaguzi kwa mfumo wa BVR kwa wilaya ya Mbinga limekamilika huku  wakazi 176744 wakiwa wamejiandikisha. Idadi hii inafanya watu waliojiandikisha kuwa ni asilimia 90 kwani idadi iliyotegemewa kujiandikisha ilikuwa ni 196110.

Zoezi la uandikishaji lilifanyika kwa awamu nne na kila awamu(zone) uandikishaji ulifanyika kwa siku 7. Wilaya ya Mbinga ina kata 43 na vituo 241. Idadi kubwa ya watu walijitokeza katika kata za Mbinga mjini,

Chanagamoto:
Uandikishaji wa watu kwa mfumo wa BVR ni teknolojia mpya kwa sehemu kubwa ya nchi yetu, hivyo moja ya changamoto wakati wa uandikishaji ni pamoja na ugumu kwa baadhi ya waandikishaji, mashine za BVR pia zilikuwa zinasumbua( Umeme na Mfumo) kwani baadhi ya watu mashine zilikuwa zinashindwa kutambua alama za vidole.

Changamoto nyingine ni kuwa watu wengi kujitokeza siku za mwisho, ni kama utamaduni wetu sisi waafrika kutojali muda hata ka vitu mhimu vya kitaifa, Uwezo wa mashine isuposumbua kwa siku ni kuandikisha watu 200 sasa vituo vingi watu walijitokeza mwishoni na hivyo kusababisha foleni kubwa.

MAFANIKIO
 Zoezi la uandikishaji limefanikiwa kwa aslimia kubwa kwani asilimia 90 ya watu waliotegemea kuandikishwa walifanikiwa kujiandikisha, mafanikio haya yalitokana sababu kuu tatu

 1.Uwezo wa waandikishaji(BVR OPERATORS) kuwa na uwezo mkubwa wa kutumia              mashine za kompyuta.

2.  Mafundi (IT TECHNICIAN) walifanya kazi usiku na mchana hivyo muda wote vituo vilikuwa          vinafanya kazi ya uandikishaji.

3.  Umeme wa uhakika , Wilaya katika kuhakikisha kuwa zoezi linafanyikiwa , ililazimika  kununua      majenereta ili kwa maeneo ambayo yanapata jua kwa kiwango cha chini kuweza kuchaji mashine       kwa  majenereta

Wilaya inatoa pongezi kwa watu wote waliosaidia zoezi la uandikishaji kufanyika kwa amani na kwa mafanikio makubwa.


No comments:

Post a Comment