Afisa miradi wa Ubalozi wa Japani Wada Anatsuki, ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na kukagua ujenzi wa Hosteli ya Namswea. .Ziara yake ilikuwa na dhumuni la kuona miradi mbali mbali ya kijamii na kimaendeleo.
Afisa miradi wa Ubalozi wa Japani,Wada Anatsuki akikagua hosteli iliyojengwa kwa ufadhili wa serikali ya Japani katika sekondari ya Namswea iliyopo Wilayani Mbinga.Ubalozi wa Japani walifadhili ujenzi wa Hosteli ya Wasichana ya shule ya Sekondari Namswea, hosteli hiyo ilikamilika mwaka jana (2014) na inauwezo wa kulaza wanafunzi 60. Hosteli hiyo iligharimu milioni 260,450,4459/= Gharama hii inajumuisha Msaada toka Ubalozi wa Japani 188,106,345/= , Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Tsh 58,109,974/= na juiya ya Wananchi wa Namswea walichangia Tsh 14,234,140/=
Katika ziara yake, Afisa Miradi huyo aliahidi kujenga tena Hosteli katika shule ya Sekondari Litembo baada ya kukagua miundo mbinu ya shule hiyo, Aidha shule ya Litembo ipo katika kata ya Litembo na inajumuisha vijiji sita. Wanafunzi wanatembea zaidi ya wastani wa Kilometa 8. Afisa miradi huyo alisema ameguswa sana na maendeleo ya wananchi wa Litembo na kutokana na maombi ya wananchi hao yalio wasilishwa ubalozi wa Japani na Diwani wa Litembo Bwana Altho Hyera.
KARIBU LITEMBO: Mkuu wa shule ya sekondari ya Litembo akimkaribisha Afisa miradi wa Japani- Ruvuma Bi. Wada Anatsuki,Afisa miradi kaahidi kuchangia ujenzi wa Hosteli ya wasichana katika sekondari hiyo.Diwani wa Kata ya Litembo akikabidhi zawadi zilizo tengenezwa na wajasiliamali wa Litembo. Diwani wa Litembo amekuwa chachu kubwa ya maendeleo kwa wakazi wa Litembo.
KILIMO
Mbinga ni moja ya Wilaya zinazoongoza kwa Ulimaji wa zao la Kahawa,Afisa miradi wa Japani -Ruvuma, Bi Wada Anatsuki alitembelea shamba la kahawa la Bwana Ernest Komba wa Utiri na kujionea wakulima wakahawa wanavyoweza nufaika na kilimo hicho.
KAHAWA:
Afisa miradi wa ubalozi wa Japani akitembelea kiwanda cha Kahawa cha MCCCO,ameahidi kutafuta wateja wa Kahawa ya Mbinga
Afisa miradi wa Ubalozi wa Japani akipata maelezo toka kwa Afisa Masoko wa kiwanda cha Kahawa cha MCCCO, Bwana Haule
No comments:
Post a Comment