HALMASHAURI YA MBINGA NA MIKAKATI YA
KUTATUA CHANGAMOTO YA MADAWATI
KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Wilaya ya mbinga ina jumla ya wakazi ………………. Ambao wengi wao
hujishugulisha na shughuli za kilimo na ufugaji. Wilaya ina halmashauri Mbili
yaani mbinga mjini na Mbinga Vijijini. Wilaya ina jumla ya kata 49(29 –Vijijini
na 19 Mjini)
Wilaya ina jumla ya shule za sekondari 58(shule za serikali
39 na za watu binafsi 19) Na shule za msingi ……. . Jumla ya wanafunzi kwa shule
za msingi ni ……..na sekondari ni …….. Maendeleo kitaaluma ni mazuri kwani
kimkoa matokeo ya mwaka 2015 imekuwa ya kwanza.Jumla ya wanafunzi 835 Wanategemewa kujiunga
na kidato cha tano kwa mwaka huu.
Wilaya inakabiliwa na changamoto ya madawati, shule za msingi
zinaupungufu wa madawati 8152 na sekondari madawati 4500, katika kukabiliana na
hilo wilaya imeanzisha karakana maalum kwa kutumia wataalamu wa ujenzi na
kuanza kuzalisha madawati kwa mapato ya ndani.
Tayari madawati 467 na viti 751 vimetengenezwa na kusambazwa katika
shule za msingi, baadhi ya shule za
msingi ambazo tayari zimenufaika na madawati haya ni pamoja na Mkinga,Kimbarakata,Mahela,MtazamaGama,Kihereketi,Luhagara,Mtunduwaro,Burundi,Ngeruke,
Mihango,Lipumba,Lukai,Luwino,Maweni,Mkumbi,Kiwanjani,Kipika,Hagati,Mkoha,Masumuni.
Jumla ya shule za sekondari 13 zimeshanufaika na mpango huu
na nyingine zitapata madawati katika awamu inayofuatia((Nyoni,Linda,Mbangamao,Mbambi,Mkako,Kiamili,Mikalanga,Mbinga
girls,Matiri,Mkuwani,Lusetu,Mbinga day na Makita )jumla ya madawati 467 na viti
751 vimegawanywa katika sekondari hizo. Pia madawati 300 yapo katika hatua za
mwisho. Halmashauri inakaribisha wahisani na mashirika mbalimbali kuchangia fedha
na fivaa ili kupunguza tatizo hili ili kufanya watoto wasome katika mazingira
bora zaidi na hivyo kuongeza ufaulu.