Thursday 14 December 2017

KUITWA KWENYE USAILI

OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA INAPENDA KUWATANGAZIA KUWA KUTAKUWA NA USAILI SIKU YA TAREHE 18–20/12/2017 KUFUATIA TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MTENDAJI KIJIJI DARAJA LA III NA DEREVA – II LILILOTOLEWA TAREHE 28/09/2017 NA 23/11/2017.

KADA ZITAKAZOHUSIKA KATIKA USAILI HUO NI WATENDAJI WA VIJIJI – III NA DEREVA II KAMA ILIVYOTANGAZWA  AWALI, USAILI UTAFANYIKA OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA KWA TAREHE TAJWA HAPO JUU KUANZIA SAA 2:00 ASUBUHI.TAREHE 18/12/2017 UTAFANYIKA USAILI WA KUANDIKA NA TAREHE 19 HADI 20/12/2017 UTAFANYIKA USAILI WA MAHOJIANO KWA WALE WATAKAOFAULU USAILI WA KUANDIKA (MTIHANI WA MCHUJO).

TAFADHALI FIKA NA VYETI VYAKO VYOTE HALISI  (ORIGINALS) VIKIWEMO CHETI CHA KIDATO CHA NNE, CHETI CHA TAALUMA (CHUO), CHETI CHA KUZALIWA NA TRANSCRIPT.
KWA MADEREVA TAFADHALI MSISAHAU KUFIKA NA LESENI YA UDEREVA.ORODHA YA WALIOCHAGULIWA KUFANYA USAILI IPO HAPO CHINI YA HILI TANGAZO.



Tuesday 14 June 2016

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA KWA MIKAKATI YA KUTATUA UPUNGUFU WA MADAWATI


Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa George Mbijima akizindua mpango wa ugawaji wa madawati katika shule za Wilaya ya Mbinga; mpango huu ni utekelezaji wa agizo la mheshimiwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa John Pombe Magufuli
WILAYA ya Mbinga mkoani Ruvuma, imetenga zaidi ya shilingi milioni 475.8 kwa ajili ya  kukabiliana na upungufu wa madawati, meza na viti  kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli, alilotoa hivi karibuni wakati akiwaapisha wakuu wa mikoa  na kuzitaka halmashauri zote hapa nchini kuhakikisha zinamaliza tatizo hilo.
Aidha wilaya hiyo tayari imefanikiwa kutengeneza madawati 6,134 kati ya madawati 12,952 ambapo kwa shule za msingi madawati yaliyokamilika ni 3,634 na shule za sekondari 2,500 sawa na asilimia 47.6 ya lengo kwa gharama ya shilingi milioni 169 na tayari yamekwisha sambazwa kwenye shule husika, huku mchakato wa kumaliza madawati 5,510 kwa shule za msingi 3,810 na sekondari 1,700 ukiwa katika hatua ya mwisho kukamilika kwake.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga vijijini, Venance Mwamengo wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa, George Mbijima katika kijiji cha Mbuji kata ya Mbuji wilayani humo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa,  George Mbijima akiangalia ubora wa meza na madawati juzi katika kijiji cha Mbuji wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma kabla ya kusambazwa katika shule mbalimbali za msingi na sekondari wilayani humo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi mtendaji alieleza kuwa kiasi hicho cha fedha ni gharama za kununulia mashine za kuranda, kukata na kukunja vyuma, mashine za kupasulia mbao, umeme na gharama zingine ndogo ndogo na kwamba madawati hayo yametengenezwa kwa kutumia mbao pamoja na chuma ili yaweze kuwa imara tofauti na madawati yanayotengenezwa kwa mbao tupu, ambayo huharibika kwa haraka na hayadumu kwa muda mrefu.

Mkurugenzi mtendaji alisema kuwa wilaya hiyo yenye halmashauri mbili ya Mbinga mjini na Mbinga vijijini  ilikuwa na upungufu wa madawati 12,952 ambayo katika shule za msingi upungufu ulikuwa madawati 8,452 viti na meza kwa shule za sekondari upungufu ulikuwa 4,500 ambapo katika utekelezaji wa agizo la serikali walianza kutengeneza madawati mwezi Januari mwaka huu na kwamba wanatarajia kukamilisha kazi hiyo ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.
Alisema kuwa mradi wa kutengeneza madawati ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, ulianzishwa ili kutekeleza agizo la serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli katika kuhakikisha kwamba halmashauri zinapunguza kero hiyo ya upungufu wa madawati, ili kuweka mazingira mazuri ya kusomea wanafunzi na walimu kufundisha watoto wanapokuwa darasani.
Kwa upande  wake kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa George Mbijima, amewapongeza viongozi wa wilaya hiyo kutokana na jitihada wanazozifanya pamoja na ubunifu wa miradi mingi na mizuri ya maendeleo ya wananchi, ambayo  imejengwa  kulingana na thamani halisi ya fedha.
Mbijima amewataka  wananchi, watumishi na viongozi wa serikali wilayani Mbinga, kutobweteka na mafanikio waliyonayo badala yake waongeze juhudi katika kufanya kazi na viongozi kutumia muda mwingi kutatua matatizo yanayowakabili wananchi.
Katika hatua nyingine aliwaagiza wahakikishe pia wanashirikisha makundi ya vijana katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo.
“Wapeni kipaumbele vijana ili nao waweze kutambua wajibu wao, mkifanya hivi ni hatua nzuri itakayosaidia kuongeza juhudi katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili, kama vile ukosefu  mitaji kwa ajili ya  kuanzisha miradi ya kiuchumi”, alisema Mbijima.
Vilevile kiongozi huyo wa mbio za Mwenge kitaifa, amewataka wazazi na walezi wilayani humo kushirikiana na serikali katika kutatua tatizo la upungufu wa madawati kwa shule za msingi na sekondari, ili kuwawekea mazingira mazuri watoto wao wanapokuwa darasani waweze kupenda kusoma na kufanya vizuri katika mitihani yao.
Pia ameviagiza vyombo vya dola kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani wanaume wenye tabia ya kuwarubuni wasichana ambao bado wanasoma shuleni kwa kufanya nao mapenzi, kwa sababu wamekuwa chanzo kwa wasichana wengi hapa nchini kukatisha  masomo yao.

Thursday 17 March 2016


HALMASHAURI YA MBINGA NA MIKAKATI YA KUTATUA CHANGAMOTO YA MADAWATI
KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

Wilaya ya mbinga ina jumla ya wakazi ………………. Ambao wengi wao hujishugulisha na shughuli za kilimo na ufugaji. Wilaya ina halmashauri Mbili yaani mbinga mjini na Mbinga Vijijini. Wilaya ina jumla ya kata 49(29 –Vijijini na 19 Mjini)

Wilaya ina jumla ya shule za sekondari 58(shule za serikali 39 na za watu binafsi 19) Na shule za msingi ……. . Jumla ya wanafunzi kwa shule za msingi ni ……..na sekondari ni …….. Maendeleo kitaaluma ni mazuri kwani kimkoa matokeo ya mwaka 2015 imekuwa ya kwanza.Jumla ya wanafunzi 835 Wanategemewa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka huu.
Wilaya inakabiliwa na changamoto ya madawati, shule za msingi zinaupungufu wa madawati 8152 na sekondari madawati 4500, katika kukabiliana na hilo wilaya imeanzisha karakana maalum kwa kutumia wataalamu wa ujenzi na kuanza kuzalisha madawati kwa mapato ya ndani.  Tayari madawati 467 na viti 751 vimetengenezwa na kusambazwa katika shule za msingi, baadhi ya shule  za msingi ambazo tayari zimenufaika na madawati haya ni pamoja na Mkinga,Kimbarakata,Mahela,MtazamaGama,Kihereketi,Luhagara,Mtunduwaro,Burundi,Ngeruke, Mihango,Lipumba,Lukai,Luwino,Maweni,Mkumbi,Kiwanjani,Kipika,Hagati,Mkoha,Masumuni.
Jumla ya shule za sekondari 13 zimeshanufaika na mpango huu na nyingine zitapata madawati katika awamu inayofuatia((Nyoni,Linda,Mbangamao,Mbambi,Mkako,Kiamili,Mikalanga,Mbinga girls,Matiri,Mkuwani,Lusetu,Mbinga day na Makita )jumla ya madawati 467 na viti 751 vimegawanywa katika sekondari hizo. Pia madawati 300 yapo katika hatua za mwisho. Halmashauri inakaribisha wahisani na mashirika mbalimbali kuchangia fedha na fivaa ili kupunguza tatizo hili ili kufanya watoto wasome katika mazingira bora zaidi na hivyo kuongeza ufaulu.

Tuesday 8 December 2015

MBINGA YA ADHIMISHA SIKU YA UHURU KWA KUTEKELEZA AGIZO LA USAFI

Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imetekeleza agizo la usafi kwa siku ya uhuru kama lilivyotolewa na Mh. Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mheshimiwa Joseph Pombe Magufuli.
Aidha katika kufanikisha  hilo, Wilaya ilitumia mbinu shirikishi kwa kuwatumia wadau mbali mbali wakiwemo wafanyabiashara , taasisi za kifedha , mashule na vikundi mbali mbali.

Ufanya usafi kwenye mazingira yetu unafaida nyingi,kunasaidia kuepukana na magonjwa yanayotokana na uchafu. Magonjwa kama kipindu pindu , minyoo, kichocho na maralia kwani mbuu huzaliana katika mazingira ya uchafu.



 PICHA: Kijiko kilichotolewa na Kanisa Katoliki jimbo la  Mbinga Kikisaidia upakiaji wa taka taka katika roli la halmashauri  dampo la misheni.Mji wa Mbinga na vitongoji vyake umekuwa katika hali ya usafi baada ya kampeni hii ya usafi.

Friday 17 July 2015

AFISA MIRADI WA UBALOZI WA JAPANI AKAGUA MIRADI NA KUAHIDI UJENZI WA HOSTELI KATIKA SEKONDARI YA LITEMBO

Afisa miradi wa Ubalozi wa Japani Wada Anatsuki, ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na kukagua ujenzi wa Hosteli ya Namswea.  .Ziara yake ilikuwa na dhumuni la kuona miradi mbali mbali ya kijamii na kimaendeleo. 

 Afisa miradi wa Ubalozi wa Japani,Wada Anatsuki akikagua hosteli iliyojengwa kwa ufadhili wa serikali ya Japani katika sekondari ya Namswea iliyopo Wilayani Mbinga.

Ubalozi wa Japani walifadhili ujenzi wa Hosteli ya Wasichana ya shule ya Sekondari Namswea, hosteli hiyo ilikamilika mwaka jana (2014) na inauwezo wa kulaza wanafunzi 60. Hosteli hiyo iligharimu milioni 260,450,4459/= Gharama hii inajumuisha Msaada toka Ubalozi wa Japani 188,106,345/= , Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Tsh 58,109,974/= na juiya ya Wananchi wa Namswea walichangia Tsh 14,234,140/=

Katika ziara yake, Afisa Miradi huyo aliahidi kujenga tena Hosteli katika shule ya Sekondari Litembo baada ya kukagua miundo mbinu ya shule hiyo, Aidha shule ya Litembo ipo katika kata ya Litembo na inajumuisha vijiji sita. Wanafunzi wanatembea zaidi ya wastani wa Kilometa 8. Afisa miradi huyo alisema ameguswa sana na maendeleo ya wananchi wa Litembo na kutokana na maombi ya wananchi hao yalio wasilishwa ubalozi wa Japani na Diwani wa Litembo Bwana Altho  Hyera.

KARIBU LITEMBO: Mkuu wa shule ya sekondari ya Litembo akimkaribisha Afisa miradi wa Japani- Ruvuma Bi. Wada Anatsuki,Afisa miradi kaahidi kuchangia ujenzi wa Hosteli ya wasichana katika sekondari hiyo.


Diwani wa Kata ya Litembo akikabidhi zawadi zilizo tengenezwa na wajasiliamali wa Litembo. Diwani wa Litembo amekuwa chachu kubwa ya maendeleo kwa wakazi wa Litembo.

 

KILIMO

Mbinga ni moja ya Wilaya zinazoongoza kwa Ulimaji wa zao la Kahawa,Afisa miradi wa Japani -Ruvuma, Bi Wada Anatsuki alitembelea shamba la kahawa la Bwana Ernest  Komba wa Utiri na kujionea wakulima wakahawa wanavyoweza nufaika na kilimo hicho. 


KAHAWA:

Afisa miradi wa ubalozi wa Japani akitembelea kiwanda cha Kahawa cha MCCCO,ameahidi kutafuta wateja wa Kahawa ya  Mbinga 
Afisa miradi wa Ubalozi wa Japani akipata maelezo toka kwa Afisa Masoko wa kiwanda cha Kahawa cha MCCCO, Bwana Haule

Monday 8 June 2015

MBINGA YAKAMILISHA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA VITAMBULISHO KWA MAFANIKIO MAKUBWA


Msimamizi wa uchaguzi kata ya Betrehemu   (ARO KATA) , Mr Alphone Njawa akiwa kabeba BVR tayari kwa kwenda kazini wakati wa zoezi la uandikishaji wa vitambulisho yva kupigia kura 2015, Zoezi hilo kwa Wilaya ya Mbinga  limekamilika hivi karibuni

Zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya kupigia kura katika daftari la kudumu la uchaguzi kwa mfumo wa BVR kwa wilaya ya Mbinga limekamilika huku  wakazi 176744 wakiwa wamejiandikisha. Idadi hii inafanya watu waliojiandikisha kuwa ni asilimia 90 kwani idadi iliyotegemewa kujiandikisha ilikuwa ni 196110.

Zoezi la uandikishaji lilifanyika kwa awamu nne na kila awamu(zone) uandikishaji ulifanyika kwa siku 7. Wilaya ya Mbinga ina kata 43 na vituo 241. Idadi kubwa ya watu walijitokeza katika kata za Mbinga mjini,

Chanagamoto:
Uandikishaji wa watu kwa mfumo wa BVR ni teknolojia mpya kwa sehemu kubwa ya nchi yetu, hivyo moja ya changamoto wakati wa uandikishaji ni pamoja na ugumu kwa baadhi ya waandikishaji, mashine za BVR pia zilikuwa zinasumbua( Umeme na Mfumo) kwani baadhi ya watu mashine zilikuwa zinashindwa kutambua alama za vidole.

Changamoto nyingine ni kuwa watu wengi kujitokeza siku za mwisho, ni kama utamaduni wetu sisi waafrika kutojali muda hata ka vitu mhimu vya kitaifa, Uwezo wa mashine isuposumbua kwa siku ni kuandikisha watu 200 sasa vituo vingi watu walijitokeza mwishoni na hivyo kusababisha foleni kubwa.

MAFANIKIO
 Zoezi la uandikishaji limefanikiwa kwa aslimia kubwa kwani asilimia 90 ya watu waliotegemea kuandikishwa walifanikiwa kujiandikisha, mafanikio haya yalitokana sababu kuu tatu

 1.Uwezo wa waandikishaji(BVR OPERATORS) kuwa na uwezo mkubwa wa kutumia              mashine za kompyuta.

2.  Mafundi (IT TECHNICIAN) walifanya kazi usiku na mchana hivyo muda wote vituo vilikuwa          vinafanya kazi ya uandikishaji.

3.  Umeme wa uhakika , Wilaya katika kuhakikisha kuwa zoezi linafanyikiwa , ililazimika  kununua      majenereta ili kwa maeneo ambayo yanapata jua kwa kiwango cha chini kuweza kuchaji mashine       kwa  majenereta

Wilaya inatoa pongezi kwa watu wote waliosaidia zoezi la uandikishaji kufanyika kwa amani na kwa mafanikio makubwa.